Thursday, September 11, 2014

IPTL YAMDAI ZITTO KABWE FIDIA YA SH. BILIONI 500


Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakimtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe awalipe fidia ya Sh bilioni 500 kutokana na kutoa kashfa dhidi yao.

IPTL, Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Harbinder Seth wamefungua kesi dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics.
Washitakiwa wengine wameshitakiwa kwasababu  makala yenye maneno ya kashfa na kuwachafua, iliyochapishwa Agosti 13 mwaka huu katika ukurasa wa 7 na 14 wa gazeti lao, ikiwa na kichwa cha habari  cha “Fedha za IPTL ni Mali ya Umma” na Kampuni ya Flint Graphics kwa kuchapisha gazeti hilo.
Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru makala hayo, yalikuwa ya upotoshaji na kuwachafua kwa kudhamiria,  pia wadaiwa waombe radhi kwa kuchapisha habari ya kuomba msamaha kwenye kurasa za mbele katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo. 

Wadaiwa hao waliiomba Mahakama, itoe zuio kwa wadaiwa, watumishi wao, wafanyakazi, washirika, wawakilishi au watu wengine wanaofanya kazi chini ya wadaiwa,  kuchapisha au kuandika makala yoyote ya kuwachafua.

UKAWA WAMVAA RAIS KIKWETE TENA


 
       SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA  kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977, 
           Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi,
              Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya  viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.

           Ambapo naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi  Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na  yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
               “Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
   Dokta Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma za watanzania kwani anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye bunge hilo  laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
           “Huyo ni Rais gani huyo ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma watazania wanaoteseka tena hata kula  mlo moja kwa siku ni kazi,yeye anakubaliana na wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli ndio kiongozi huyu,kwasababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha za Chache kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake”alizidi kusema Dokta Slaa.
        Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili  Rais ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
        “Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo wate maanuzi tulitofikia katika mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana kuhailisha mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja ahamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia ujinga huo”alisema Mbatia
         Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge hilo Maalum la katiba aliongeza kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema  Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
          Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
         “Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi  kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema profesa Lipumba.
   Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia merekebisho katiba iliyopo?
    Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete asipofanyia marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti kubwa na  ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa sana kwani Umoja huo hautokubaliana na yeye.

       Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata Fursa hiyo.

MTANZANIA APEWA CHEO BET


Kabla ya kuanza kukupa info kuhusu huyu Mtanzania nataka nikukumbushe headlines chache za Watanzania walioingia kwenye headlines za kimataifa hivi karibuni.
Ni CloudsTV International kufungua ofisi Kingston Jamaica ambayo itahudumia ukanda wa Caribbean, Diamond Platnumz kuchaguliwa kushiriki tuzo za MTV Europe, AzamTV kuanza kufanya kazi Uganda kwa kuhudumia mamilioni kupitia king’amuzi chake na power bank za Puku zinazomilikiwa na Mtanzania aishie Marekani.
Sasa hivi vichwa hivyo vya habari vitaongezewa hii kubwa nyingine baada ya Mtanzania Kay Madati kuchaguliwa kuwa makamu wa Rais katika kituo kikubwa cha Television nchini Marekani BET.

Taarifa iliyoandikwa na Mtandao maarufu wa Forbes imesema amechaguliwa ‘Kay Madati as Executive Vice President and Chief Digital Officer. Madati, a Tanzanian citizen who has lived in Africa, the United Kingdom, and the United States’
Nilikua sifahamu kama Madati ambae ni raia wa Tanzania aliyeishi UK, Marekani na Afrika, aliwahi kuwa makamu wa Rais CNN Worldwide… aliwahi pia kufanya kazi na BMW Amerika kaskazini, Octagon Worldwide lakini pia amefanya kazi na Facebook.
‘Madati was most recently the Head of Entertainment and Media on the Global Marketing Solutions team at Facebook Inc‘
Sehemu ya kazi ya Madati BET itakua ni kuziongoza timu za BET kwenye maswala ya digital ‘will oversee BET Digital, the interactive arm of BET Networks whose platforms include BET.com, which encompasses entertainment, music, culture, and news; BET Mobile, which provides apps, ringtones, games and video content for wireless devices; Centric.tv, the online home for the Centric cable channel; and BET Video On Demand, one of the largest VOD services providing African-American content‘

ALIYEDAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA POLISI, UKWELI WAJULIKANA


Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Liberatus Damiani Temu (55) anayedaiwa kufariki kiutata.
 KIFO cha mfanyabiashara aliyeshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, Liberatus Damiani Temu (55) kilichodaiwa kilitokana na kipigo kutoka kwa askari wa kituo hicho sasa ukweli umejulikana.Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa utata wa tukio hilo ulianzia mbali kwani Mei, mwaka huu, marehemu alimgonga na gari mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis Magoma na kujeruhiwa vibaya.

Mke wa marehemu, Naomi Liberatus (katikati) akihuzunika kwa kumpoteza mwenzake.
 Baada ya kusababisha ajali hiyo, ilidaiwa marehemu Liberatus alifuatilia masuala ya bima ili aweze kumlipa aliyemgonga ambaye pia anatajwa kuwa mteja mzuri katika Baa ya Meku iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu.
Naomi Liberatus akiwa amezimia wakati wa mazishi.
Chanzo kinasema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, hali ya Magoma iliendelea kuwa mbaya hadi Agosti 22, mwaka huu saa tano usiku marehemu alipokamatwa na kufikishwa kituoni hapo akidaiwa kumjeruhi Magoma kwenye ajali.
Padri akiiombea roho ya marehemu ya marehemu (Liberatus Damiani Temu).
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus aliyezimia mara mbili wakati wa mazishi, alisema mumewe ambaye kwa kipindi chote tangu apate ajali hiyo, alikuwa hafanyi shughuli yoyote, alikataliwa kupewa dhamana kwa madai kuwa majeruhi (Magoma) alikuwa na hali mbaya.
Mwili wa marehemu Liberatus Damiani Temu ukichukuliwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
Kuhusu hatua nyingine ilidaiwa kuwa marehemu akiwa mahabusu aligonga kichwa chake kwa nguvu ukutani, hali iliyosababisha wenzake kupiga kelele za kuomba msaada na kwamba baada ya askari kufika na kukuta hali ilivyo, walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu ambako alifariki dunia.
Marehemu Liberatus Damiani Temu enzi za uhai wake.
 “Watu wanasemasema tu kwamba Liberatus aliuawa na askari, si kweli. Kwa nini tumuue? Kwa kosa lipi? Sisi tulimshikilia kwa sababu hali ya majeruhi aliyemgonga ilikuwa mbaya, hivyo kumweka mahabusu marehemu ilikuwa kwa ajili ya usalama wake pia.

KIJANA AUAWA AKITUHUMIWA USHIRIKINA MKOANI MBEYA

 Marehemu akipakiwa kwenye gari tayari kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti.

Ndugu na jamaa wakishiriki maziko ya marehemu, Gabriel Mwasyebule kijijini kwao ndembo lwangwa.
Marehemu Gabriel Mwasyebule enzi za uhai wake.
Nyumba ya marehemu, Gabriel Mwasyebule anayotuhumiwa kuijenga kwa uchawi.
Moja ya shamba la viazi vinavyo subiriwa kuvunwa mwezi huu, shamba la marehemu, Gabriel Mwasyebule, mashamba amabayo pia ni moja ya sababu ambazo wananchi wa lwangwa wanamtuhumu marehemu kuwa alikuwa anawalimisha watu kiuchawi na kuiba mazao ya mashamba mengine kiuchawi ili shamba lake liwe na mazao mengi na mazuri.
Hii ndio stoo kuwekea mazao mbalimbali ambayo marehemu alikuwa anatumia kutunzia mazao yake.
MATUKIO ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio hili kijana Gabriel Mwasyebule miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu aliyetambulika kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande (Lwangwa) Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.

Alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya

Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.

Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi ya mavuno ya viazi na kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka marumaru na Gipsam pia kumiliki pikipiki moja huku akitarajia baada ya mavuno mazuri ya mwaka huu kununua gari la kutembelea.

Tuesday, September 9, 2014

RAIS KIKWETE AHITIMISHA MAZUNGUMZO YAKE NA UJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA IKULU NDOGO DODOMA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU.

WATAWA NA MAAJUZA WABAKWA MPAKA KUFA

Maafisa wa kanisa wanasema kuwa watawa hao waliuawa na mhali mwenye akili pungwani
Watawa watatu wakongwe wamebakwa na kuuawa mjini Bunjumbura katika makazi ya watawa wanawake viungani mwa mji mkuu huo.
Sababu ya mauaji hayo haijulikani. Polisi wanasema kuwa wamewazuilia washukiwa wawili, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Watawa hao walisemekana kuwa Lucia Pulici,mwenye umri wa miaka 75, Olga Raschietti, 82 na Bernadetta Boggian, 79.
Wawili kati ya waathiriwa, waliuawa Jumapili huku mwili wa mwingine wa tatu ukipatikana Jumatatu ukiwa umekatwakatwa.
Maafisa wakuu wanasema kuwa mshukiwa wa mauaji hayo, alionekana akitoroka makazi ya watawa hayo akiwa ameshika kisu mkononi
Dayosisi ya Italia ya Parma inasema kuwa watawa hao waliuawa wakati wa jaribio la wizi katika makazi yao.
Hata hivyo haijulikani kwa nini watawa hao waliuawa kwani hakuna kilichoibwa kutoka kwao.
Watawa hao wawili walikuwa wanashiriki katika kanisa katoliki la Xaverian.Kwenye mtandao wake, dayosisi ya kikatoliki ya Parma ilisema kuwa mauaji ya watatu hao yalifanywa na mhalifu ambaye alikuwa na matatizo ya kiakili.
Mnamo mwaka 2011,mtawa mmoja na mfanyakazi wa shirika la misaada aliuawa katika tukio la ujambazi Kaskazini ya Burundi
Burundi ni moja ya nchi masikini ambapo uchumi wake unategemea sana mapato kutokana na Chai na Kahawa zinazouzwa nje