Thursday, September 18, 2014

MASKINI NDOA HII JAMANI IMEFIKIA HAPA

Stori: Richard Bukos
PAMOJA na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.

Tukio hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.

WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu,  baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.

JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.

WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda  kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.

MAPACHA WALIOUNGANA MWILI WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE KUHITIMU KIDATO CHA NNE MWAKA HUU



Hatua ya kwanza ya ndoto ya kuzama katika elimu ya mabinti pacha walioungana kiwiliwili, Consolata na Maria Mwakikuti (18) wa Kijiji cha Ikonda wilayani Makete  mkoa mpya wa Njombe, inatarajiwa kutimia Novemba mwaka huu, wakati mabinti hao watakapofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.
 
Itakumbukwa kwamba walipokuwa wakimaliza elimu ya msingi mwaka 2009 kijijini kwao Ikonda, walikuwa na umri wa miaka 13 na katika ndoto zao kwa pamoja walisema wanataka kuwa wasomi waliobobea katika utaalamu wa kompyuta. Lakini, kwa sasa, wanasema wanatamani kufanya kazi ya Ukatibu Muhtasi.
 
Wanafunzi hao mwaka 2010 walichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, Dar es Salaam.
 
Kwa sasa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Maria Consolata iliyopo Kidabaga wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Shule hiyo inamilikiwa na Kituo cha Nyota ya Asubuhi ya Wamisionari Wakatoliki wa Italia, kinachosaidia kuwatunza watoto wanaotoka katika mazingira magumu.
 
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii shuleni hapo hivi karibuni, walisema wanafurahi kuwa miongoni mwa watahiniwa watakaofanya mtihani huo wa kidato cha nne mwaka huu.
 
"Tunafurahi, tunajiandaa tunasoma kwa bidii, mtihani uko karibu tunataka tufaulu vizuri masomo yetu, ili ile ndoto yetu ya kuwa Makatibu Muhtasi itimie," walisema Maria na Consolata, ambao wanatumia baiskeli maalumu kuwapeleka darasani, ambako pia wana kiti maalumu.
 
Pacha hao wameshangaza watu wengi kwa jinsi walivyo, ambapo kila mmoja ana madaftari yake. Wakati wa kufanya mazoezi au kuandika kazi wanazopewa, mmoja huanza kuandika, akimaliza na mwingine huandika.
 
"Wala hatupati shida tumezoea, kila mmoja anafanya kazi yake, mimi naandika kwa mkono wa kushoto na Maria anaandika kwa mkono wa kulia," anasema Consolata, ambaye anaonekana kuwa mchangamfu zaidi.
Shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Ilianzishwa mwaka 2006 na hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 183. Wote wanaishi kituoni hapo na wote wanatoka kwenye mazingira magumu.
 
Changamoto kubwa iliyokuwa shuleni hapo ni ukosefu wa nishati ya umeme, ambapo uongozi wa shule na kituo hicho unalazimika kutumia jenereta na umemejua, jambo ambalo mapema wiki hii Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA), imewaondolea adha kwa kuwapelekea umeme.
 
Pacha hao walizaliwa mwaka 1996 wakiwa wameungana katika Hospitali ya Ikonda wilayani Makete mkoani Iringa.
 
Walifaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2010, ambapo kila mmoja alipata alama 151, ingawa walitofautiana ufaulu  kwenye masomo yao.
 
Katika somo la Maarifa ya Jamii, Consolata alipata alama 29 na Maria alama 25, kwenye somo la Kiingereza, Maria alipata alama 36 na kumzidi Consolata aliyepata alama 34, wakati kwenye somo la Sayansi, Maria alimzidi Consolata kwa kupata alama 31 dhidi ya 29.
 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliwapanga pacha hao kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam.
 
Hata hivyo hawakujiunga na sekondari hiyo, kutokana na hali yao na pia umbali kutoka Iringa hadi Dar es Salaam. Ndipo Wamisionari hao wakawachukua mwaka 2011 na kuanza kidato cha kwanza.
 
Walizaliwa kwenye Hospitali ya Misheni ya Ikonda mwaka 1996. Lakini, taarifa zao hazikufahamika hadi pale walipoandikishwa kuanza elimu ya msingi Ikonda na kutafutiwa mlezi wa kuwaangalia, baada ya wazazi wao kufariki dunia wakiwa bado wadogo.

UBAGUZI WA RANGI WAZIDI KUTIKISA ULIMWENGU WA SOKA

Na Saleh Ally
WAKATI mwingine nimekuwa najiuliza mambo maswali mengi sana kuhusiana na suala la ubaguzi wa rangi ambalo linaonekana wakati mwingine kulielemea Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Nianze na mkasa wa juzi ambao umemtokea kiungo nyota wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ambaye hivi karibuni amejiunga na klabu ya Querétaro ya nchini Mexico ambako anaamini ndiyo atamalizia mpira wake.
Ronaldinho amebaguliwa, amedharauliwa na kuitwa sokwe, licha ya kwamba hakuwa na kosa hata punde.
Aliyembagua ni mwanasiasa maarufu wa chama kinachojulikana kama National Action Party (Pan) ambaye pia amewahi kuwa waziri wa serikari ya Mexico.
Jamaa anaitwa Carlos Manuel Treviño ambaye ameingia kwenye kundi la wapuuzi na wajinga wanaoamini ubaguzi wa rangi ni nyenzo.




Kisa cha kumbagua Ronaldinho ni kwa kuwa mwanasiasa huyo alikuwa akitokea katika mihangaiko yake anarejea nyumbani, kukawa na foleni kubwa sana njiani na mwisho aligundua inatokana na mashabiki wa klabu ya Queretaro waliokuwa wakitokea kwenye Uwanja wa Corregidora kumpokea kiungo huyo alipokuwa anatambulishwa.
Akaamua kuweka maneno ya kashfa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akimuita sokwe ambaye amesababisha yeye kuchelewa kufika nyumbani.


Mpira ni burudani kubwa lakini ni chombo bora kabisa cha kuwaunganisha watu mbalimbali wakiwemo wale waliogombana, wasiopendana au kutoelewana.
Nchi nyingi zilizoingia kwenye vita hasa vile vya wenyewe kwa wenyewe, mwisho zimetumia nguvu zaidi kwenye mchezo wa soka ili kurejesha hali ya utulivu.
Mfano mzuri ni Wanyarwanda ambao baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994, soka ndiyo chombo kilichosaidia kwa asilimia kubwa kuwaunganisha, pia kujitahidi kusahau mabaya na makali yaliyopita.

Sasa jiulize, wakati wengine wanatumia soka kama chombo unganishi, vipi hao wanatumia mchezo huo kama chombo tenganishi kwa lengo la kudharau, kuonea au kubeza bila hata sababu yoyote ya msingi.
Ninazungumzia Wazungu, ninazungumzia watu weupe wanaoamini ni bora kuliko Weusi hata kama heshima yao haiko juu kama wanavyofikiri.
Wakati mwingine unaweza kufikiri hata wao Fifa ni wababaishaji kwenye hili kwa kuwa hakuna adhabu kali zaidi kwa wanaofanya hivyo viwanjani.
Kuna kila sababu ya kuliangalia zaidi kwa kuwa wale wanaowabagua weusi, wanakuwa hawana heshima ya kimatendo au hata fedha dhidi yao.
Angalia waliombagua Samuel Eto’o au Yaya Toure kule Urusi. Mfano mwingine wale mashabiki ambao huwabagua wachezaji Waingereza au kule Hispania.
Ajabu hili linafanywa hata na wachezaji kwa wachezaji, nafikiri ndiyo ungekuwa mfano mzuri zaidi kuwaonya wabaguzi wengine.
Ikitokea mchezaji kambagua mwenzake, halafu ushahidi ukawa umepatikana kwa uhakika, basi afungiwe msimu mzima.
Wale mashabiki wanaweza kujifunza kupitia adhabu kali ambazo watapata wachezaji, makocha, viongozi na hata waamuzi ambao wataonyesha ubaguzi.
Nani kasema ngozi nyeupe au ngozi ya mzungu ndiyo akili? Upuuzi mtupu!
Tunajua Fifa ina Wazungu wengi kuliko Weusi, huenda linaonekana si suala kubwa sana na mapambano yake yako kwenye mapango tu bila ya vitendo.
Huenda adhabu ingekuwa kali sana kama Waafrika wangekuwa na nafasi ya kuwabagua Wazungu pia. Fifa bado inahusika na inapaswa kujua upole wake katika hilo, unazidi kufanya liendelee.
Wazungu wanaobagua Weusi ni wapuuzi, Fifa haipaswi kuacha upuuzi huo uendelee kwa kuwa si Weupe tu ndiyo wanaoujua kuucheza mpira na mfano mzuri wa kuwa Weusi wanaujua mpira, jikumbushe kwa Pele.
Wajinga kama mwanasiasa yule wa Mexico aliyembagua Ronaldinho ambaye sasa tayari yuko katika hali mbaya kisiasa kutokana na kusakamwa sana na mashabiki wa soka, wanapaswa wapate joto ya jiwe kama anayokutana nayo, la sivyo hawataacha.
Lakini kwa Fifa na mashirikisho ya soka Ulaya, nayo yapambane kuzuia hilo kwa kuwa inakuwa ajabu, hata Wazungu wenye njaa, nao wanawadharau Waafrika wenye mafanikio zaidi eti kisa ni Weupe. Huu ni upuuzi mkubwa.

MTOTO ALIYEZAMIA NDEGE: ATOWEKA TENA



Mtoto Happiness Rioba(10) aliyedaiwa kuzamia kwenye ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kugundulika, ametoweka tena nyumbani kwao baada ya kukutanishwa na mama yake mzazi Sara Zefhania.

Happiness ambaye ni mkazi wa eneo la Mkokozi, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani inadaiwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na Mwananchi jana, Sara alisema mwanawe alitoweka jana saa sita mchana na kutokomea kusikojulikana.Alisema asubuhi mtoto wake aliamka salama bila tatizo lolote na muda wote walikuwa pamoja kwa kuwa alikuwa na wageni kutoka kituo cha televisheni cha ITV, waliomuahadi kumtembelea nyumbani kwa lengo la kumuona Happiness.

“Aliamka vizuri tu na muda wote alikuwapo nyumbani, lakini ilipofika saa sita mchana, nilipigiwa simu na waandishi wa habari wa ITV kuwa nikawachukue katika kituo cha daladala... kabla sijaondoka nilimwambia mwanangu nakwenda kupokea wageni, lakini niporejea nyumbani na wageni hatukumkuta,” alisema Sara.

Alisema baada ya kumkosa alianza kumtafuta akishirikiana na waandishi hao pamoja na majirani, lakini hawakufanikiwa kumpata ndipo alipotoa taarifa kwa mjumbe wa Serikali za Mitaa na kuwataarifu ndugu, jamaa na marafiki.

Aidha, aliongeza mwanawe alipokuwa Zanzibar alifanya mambo ya ajabu likiwamo kuongea na paka, kula chakula kwa kutumia mkono wa kushoto, kutokuongea na watu pamoja na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Alifafanua kuwa walipofika nyumbani wakitokea Zanzibar alianza kumdadisi kutaka kujua alifikaje huko na je kweli alipanda ndege, alisema baba yake ndiye alimuita ili akaishi naye huko.

CHAMA CHA ZITTO KABWE ACT,CHAFUNGUA OFISI ZILIPO OFISI ZA CHADEMA ARUSHA...


MAMA NA MWANAYE WAOANA BAADA YA KUWA NA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA



"Mimi na Vertasha mwanangu tulianza mahusiano yetu wakat kipindi hicho akiwa na miaka 16 tu.Lakini nilisubiri mpaka afikishe miaka 18 ndipo tungeanza mapenzi kabisa kwa sababu ni umri ambao unaruhusiwa kisheria,sasa tunatembea out bila kificho chochote ili kuwa saidia watu wengine ambao wako kwenye uhusiano wa kishoga/mama na mwana/wasagaji ilio wajisikie huru.Tunataka watu watutambue kwamba sisi tuna mahusiano ya jinsia moja kama kawaida alisema mama huyo"

Sheria zinazuia mahusiano ya kindugu hasa suala la usagaji katika nchi nyingi za kiafrika..
 "Sisi ni wanawake kwa hiyo mimi Vertasha hatuwezi kuzaa watoto tena na tumeridhika na mahusiano yetu "

Vertasha anafurahia mahusiano hayo pia na anasema hivi...!!

"Mama yangu ni mama yangu anafanya vitu ambavyo ni wajibu wa mama kuvifanya,ananinunulia nguo ananinunulia chakula ananiambia nikatandike kitanda ,so imetokea tu tukawa tunafurahia mapenzi kwa pamoja"

MAMIA WAMSINDIKIZA MBOWE POLISI

 


Ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa eneo la Makao Makuu ya Polisi wakati Freeman Mbowe akiwasili kuhojiwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), Halima Mdee akiwasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar leo.
Wananchi wakiwa Makao Makuu ya Polisi.
Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Katika tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika makao makuu hayo ya polisi.
Mmoja wa wanachama ambaye alibishana na askari na kujikuta akipata kibano kidogo na baadae kuachiwa 
Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE leo amefanya shughuli za jiji la Dar es salaam kusimama kwa muda baada ya kufika makao makuu ya polisi jijini akiwa na wanasheria wa chama huku mamia ya wanachama wake wakiwa nyuma yake kutaka kujua kinachoendelea hapo ikiwa ni kuitikia wito wa jeshi hilo waliomtaka kufika kwa maelezo zaidi.
Baada ya mh MBOWE kufika makao makuu ya polisi aliingia ndani na kuhojiwa zaidi ya masaa manne na kisha mwanasheria wa chama hicho mh TUNDU LISSU kutoka na kauli kuwa mwenyekiti huyo ametuhumiwa kuwa makosa ya uchochezi alioufanya juzi jumapili wakati akihutubia wanachama wake ambapo alisema kuwa wataandamana na kufanya migomo nchi nzima kupinga bunge la katiba linaloendelea.
Hata hivyo kwa taarifa ya TUNDU LISSU ni kuwa mh MBOWE ameachiwa kwa dhamana kwa ajili ya kusubiri kesi yake hiyo.
Hata hivyo mh MBOWE alionekana kufichwa sana kiasi cha kutoikuwa rahisi kuonekana na wafuasi wake
Nje ya ofisi za jeshi la polisi wananchi ambao ni wafuasi wa CHADEMA walionekana kuwa na hamu ya kumwona mwenyekiti wao ambapo kwa mara kadhaa walisikika wakiimba na kupiga kelele ambapo polisi walianza kuwasukuma na kusogeza silaha zo karibu ila hali ikawa shwari.hadi mtendao huu unaondoka katika eneo la tukio wafuasi hao walikuwa wameondoka kwa maombi ya mwanasheria tundu lissu kuwa waondoke hapo ili kuepusha vurugu zisizo na msingi
Viongozi wa chama hicho walikuwepo kuhakikisha kuwa hali inakua shwari 
Mh TUNDU LISSU akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari ambao aliwataka kuondoka katika maeneo hayo ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kuwaharibia zaidi katika kesi hiyo