Saturday, November 22, 2014

MAHAKAMA YAKANA KUANDIKA BARUA KUZUIA MJADALA WA TEGETA ESCROW BUNGENI

Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSeM426Cq0CaW6cLRxF3-eMk_YcC0OAnvxqPvX0QwMsgu2y2CaTM3bZXJnEvNLh7a_WJoUNhlIFtYC8nhqK13EdmpdwP_e7S9I5xF-UHM-NqKCL78XekaUd6QwtBCQwF3taWT6alG92v9i/s1600/wabunge6.JPG
Sakata hilo lililotawala kikao cha Bunge hilo jana lilitokana na madai yaliyoibuliwa juzi na wabunge wa kupinzani unaoundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi.

Wabunge hao Tundu Lissu (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Habib Mnyaa (CUF) waliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuwa wamepata taarifa za uhakika kuwa Mahakama imeandika barua ikiritaarifu Bunge lisijadili kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Wabunge hao, walisema kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Bunge na kwamba lengo lake ni kutaka kukwamisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili wahusika wasichukuliwe hatua.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.

“Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo,” alisema Msumi.

Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya serikali iliyothibitisha rasmi kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge.
Juzi Naibu Spika,Job Ndugai, alisema kuwa ofisi ya Spika haijapokea barua hiyo.

Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizungumza bungeni jana kuhusiana na madai hayo, hakuthibitisha wala kukanusha kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda bungeni kuzuia mjadala huo, zaidi ya kusisitiza itumike busara ili kuepusha mihimili hiyo kuingiliana katika majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Chanzo: Nipashe

A-Z KUHUSU BILIONEA ALIYEKUFA AKIWA NDANI YA GARI BUKOBA!


Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari. Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na kimada wake aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.

KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Bukoba kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa siku ya leo. 

Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.
“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.

 
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.

Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Binti aliyekuwa na marehemu.

Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya. 
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye madhara,” kilisema chanzo chetu.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.


Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.

 “Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo chake,  daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida. “Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa. 
“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu. 
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.

“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.

Friday, November 21, 2014

WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI...



Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge …
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo

KUNA BIASHARA YA WASANII WA KIKE WA MUVI INAENDELEA


Jokate Mwegelo akipozi.
 Stori:  Waandishi Wetu
Imefichuka! Kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa za chini kwa chini kwamba baadhi ya mastaa wa kike Bongo, hasa wale wa filamu ‘Bongo Movies’ huuzwa kwa wanaume, mara nyingine kwa kujua au kutojua lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha hivyo kutoa ‘kibarua’ kwa Ijumaa kuingia mzigoni kisha kumuibua mmoja wa wahusika (kuwadi) anayerahisisha biashara hiyo haramu ya ngono.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, kuwadi huyo huwa anajua dau la kila staa hivyo anapopata mwanaume hasa mapedeshee, wafanyabiashara na baadhi ya vigogo serikalini, huwaunganisha kwa kutoa namna ya mawasiliano au kuwaunganisha moja kwa moja.

Uchunguzi huo ulibaini uwepo wa madai mazito kwamba wapo baadhi ya mastaa wa kike wa Bongo Movies ambao hugombewa na makuwadi kwa sababu wana soko kubwa.
“Jaribu kufikiri msanii haonekani location (eneo la kuigizia sinema) wala sinema aliyocheza haijulikani lakini muda mwingi utamuona anatanua kwenye viwanja vya starehe, lazima ujiongeze kwamba kipato kinatoka wapi?
 
Staa wa filamu Bongo Aunt Lulu.
“Mimi nakwambia hii Bongo Movies imebaki jina tu, sioni mwanga mbeleni kwa sababu hawa mabinti hawapo serious zaidi ya kutafutiwa wanaume,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mfuatiliaji wa karibu wa kazi za sanaa Bongo.

Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba wapo wanunuaji ambao huhonga magari (bila kadi) ambapo baadaye hukamatwa kimafia na kurejeshwa kwa mhongaji.
Ikazidi kufahamika kwamba, mastaa wenye sifa ya kuhongwa magari ni wale wenye majina makubwa.
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe.

Ilisemekana kwamba wapo mastaa wanaotajiwa dau kubwa kuanzia Sh. milioni tano na kuendelea na wapo wa chini ya hapo hadi buku hamsini (50,000).
Mpaka sasa kuna mastaa wanaowindwa na makuwadi kwa kuwa wana soko na bei zao kwenye mabano ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ (Mil. 5), Jokate Mwegelo (Mil. 5), Wema Isaac Sepetu (Mil. 5), Kajala Masanja (Mil. 5) na Jacqueline Wolper Massawe (Mil. 5).
 
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’.
Wengine ni Baby Joseph Madaha (Mil. 5), Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ (Mil. 3), Aunty Ezekiel (Mil. 3), Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ (Mil. 2) Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ (Mil. 1), Lulu Mathias ‘Anti Lulu’ (Mil. 1), Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ (Mi. 1) na wengine kibao ambapo kwa sasa upepo umegeukia kwa wale wanaochipukia.
 
Katika kusaka ukweli juu ya skendo hiyo, jina la mmoja wa makuwadi hao ambaye ni mwigizaji wa kike Bongo, Lungi Maulanga (pichani) ilitajwa.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mbali na Lungi pia alitajwa mwigizaji mmoja wa kiume wa Bongo Movies na jamaa mwingine ambaye huwa ni mdandiaji wa ishu za mastaa (majina tunayo, tutayataja tukijiridhisha kisheria).

Baada ya kutajiwa jina la Lungi, gazeti hili lilimsaka mwigizaji huyo anayedaiwa kuwauza baadhi ya mastaa hao kwa wanaume ambapo alibanwa vilivyo hadi akaanika siri nzito nyuma ya biashara hiyo kubwa isiyo na kodi.
 
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Mbali na kukiri kuwakuwadia mastaa hao kipindi cha nyuma kabla ya kuacha, Lungi alifunguka kwamba amekuwa akisumbuliwa na wanaume wakware wakitaka awaunganishe na mastaa ambao alidai alishafanya nao kazi hiyo muda mrefu.
MSIKIE LUNGI Ijumaa: Habari yako Lungi... Lungi: Nzuri, mmekuja kufuata nini hapa (nyumbani kwake Kinondoni, Dar)? Ijumaa: Mbona unajihami? Tumekuja kukusomea mashitaka yako! Lungi: Mashitaka gani? Siku hizi nimetulia, sijichanganyi kama zamani, kulikoni tena? Ijumaa: Hapa kuna madai mazito...
 
Staa wa filamu Bongo, Vai wa Ukweli.
Lungi: Hebu semeni kilichowaleta, kwanza siku hizi sipendi kukutana na waandishi wa habari! Ijumaa: Kuna za chinichini kwamba wewe ndiye unayewauza mastaa wa Bongo na ndiyo biashara inayokuweka mjini kwa kuwa hata location huonekani. Je, ni kweli?
Lungi: (kwa hasira) yaani mimi niwekwe mjini na mastaa? Kwani hamjui anayeniweka mjini? Au mnataka niwafukuze na panga?Ijumaa: Kwa nini unakuwa mkali Lungi? Unachotakiwa kufanya ni kutoa majibu kwa sababu kuna shosti’ako ametutajia staa uliyemuuza juzi tu!
Staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel akipozi.
Lungi: (bila kujua anarekodiwa) juzi! Sikieni, nawaheshimu sana, mimi nilikuwa nikifanya biashara hiyo siku nyingi na niliacha kwa sababu hao mastaa hawana maana, wakishapata wanajisikia na kusahau walipotoka.
“Huyo aliyewaambia ana ushahidi gani kama juzi nimeshamuuza staa? Ijumaa: Oke, tuache hilo! Unakumbuka dau kubwa ulilowahi kupewa wakati unawakuwadia? Lungi: (kwa mara ya kwanza anatabasamu) nilishawahi kupata hadi Sh. milioni tatu na kima cha chini laki tano, lakini jamani mbona ni siku nyingi?
 
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
“Kwanza mimi sitaki hizo habari kabisa. Nimechoka kusumbuliwa na wanaume kwa ishu hizo.”Ijumaa: Hilo dau kubwa ulilipata kwa mwanaume wa Dar, mikoani au nje ya nchi?Lungi: Watu wa mikoani ndiyo wanakata mkwanja mkubwa, hapa Dar longolongo tu. Hiyo Sh. milioni tatu niliipata kwa jamaa mmoja wa Arusha.

KIJANA SANDE MREMI AFARIKI DUNIA,NDEGE ZILIGOMA KUMSAFIRISHA

Sande Jacob Mremi amefariki Siku chache baada ya kukosa usafiri wa ndege ambapo alitakiwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu.Kituo cha ITV kiliripoti kuhusu habari za kijana huyo kuumwa na kutokana na kusumbuliwa tatizo la uzito mkubwa nakushindwa kupata Ndege ya kumsafirisha kwenda kwenye matibabu India kijana huyo amefariki Dunia.Ndugu wa kijana huyo walilalamika kutoridhishwa na baadhi ya Mashirika ya Ndege kwa kushindwa kuwasaidia kumsafirisha ndugu yao.Katika mahojiano na ITV mama wa mtu huyo amesema; “..yaani kwa kweli mashirika ya Ndege hayakuweza kutufanyia haki kwa kweli, wametunyanyasa kwa sababu tulipokuwa tunapeleka maombi tunataka kumsafirisha mtoto wetu ilikuwa wao watusaidie na kutupa maelekezo tunatakiwa tufanye nini na nini, lakini baada ya kuona tunakosa msaada ndio tukaamua kuja ITV ili watusaidie, kwa hiyo yeye mwenyewe akaanza kupata presha kwa sababu presha alikuwa hana mpaka anapanga kusafiri alikuwa hana presha nilimpima vipimo vyote alikuwa hana tatizo lolote…”

Dada wa marehemu amesema; “..Ethiopia walitusaidia kwa kweli mpaka hatua ya mwisho na Jumapili kama Mungu angemuweka hai Ethiopia wangemsafirisha, na mashirika ya Ndege mengine yalitakiwa yatuelekeze hivi, lakini sasa kutokana na ile hali mara leo kapelekwa kesho anarudishwa mdogo wangu kesho kutwa kapelekwa amerudishwa mdogo wangu, msongo wa mawazo umemkaa rohoni anashindwa kuongea maskini ya Mungu, mawazo paka yamemfanya mdogo wangu alikuwa hana presha paka presha imekuja paka mdogo wangu anafariki.
sds
Baba wa Sande amesema; “…wakatumia sheria ya pili ya kunihusisha mimi wakaniambia bwana kumbe mtu huyu ni mkubwa sana tunatakiwa tuvunje viti tumbebe, nikawauliza nikulipeni bei gani? wakaniambia tulipe dola elfu saba mia tano na thelathini na nne, na mara ya kwanza tulilipa dola elfu sita miambili ishirini…”
Bado haijafahamika kama Shirika hilo la ndege litarudisha hela ambayo ililipwa na watu hao kwa ajili ya kumsafirisha ndugu yao.

WABUNGE WACHARUKA KASHFA AKAUNTI YA TEGETA-ESCROW

Hawa ndio wabunge waliofunguka wakitaka sakata hilo lijadiliwe bungeni
Naibu spika wa bunge Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la"
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti nya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, (CHADEMA),akizunghumza bungeni mjini Dodoma jana, wakati lile sakata la IPTL, linalogubigwa na akauti iliyojichukulia umaarufu TEGETA ESCROW, lilipoibuka bungen i wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu. Wabunge wanataka "ngoma" ijadiliwe bungeni, licha ya kashfa hiyo kuwa tayari mahakama kuu ya Tanzania
Mbunge wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, huyu ndiye aliyeibua kashfa ya akaunti ya Tegeta-Escrow
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mbunge wa Urambo, (CCM), Samwel Sitta
Mbunge wa Iringa mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-M,ageuzi, James Mbatia
Mbunge kijana, Esther Bulaya, (CCM)
Mbunge wa Longido,(CCM), Lekule Laizer,
Mbunge wa Kasulu mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ndiye aliyemchokoza Waziri mkuu kuhusu ripoti hiyo kujadiliwa bungeni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, "Punguzeni jazba", akiwasihi wabunge kuwa serikali iko makini na inasubiri kwa hamu taarifa hiyo ili kila mtu hata yeye akibainika abebe msalaba wake, lakini akatahadharisha kuhusu umuhimu wa kuheshimu mihimili ya dola ikiwemo mahakama
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli

LORI LALIPUKA ENEO LA MIKUMI MKOANI MOROGORO


 Tumepokea picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi, Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wetu  alietuletea taswira hizi kuhusiana na hali ya barabara hiyo.
''Kama una safari ya kwenda Iringa-Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi basi sitisha safari kwani njia inefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado inawaka na inesambaa sehemu kubwa''
Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo la ajali.