JUMBA lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya washiriki wa shindano la Big Brother Africa (BBA)
2014 limeteketea kwa moto jana eneo la Sesani Studios jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Septemba 7, mwaka huu.
Katika taarifa iliyotolewa na waandaaji wa shindano hilo, M-Net na Endemol ni kwamba katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo chake.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa sasa linatafutwa jumba lingine litakapoendeshwa shindano hilo linalochukua siku 91.
No comments:
Post a Comment