Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa
Maafisa wakuu kutoka shirika la
polisi wa kimataifa, Interpol amethibitisha kuwa gari la ulinzi wa rais
Uhuru Kenyatta lililoibwa mjini Nairobi wiki jana limepatikana nchini
Uganda.
Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Gari
hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini Nairobi. Watu
watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.Mkurugenzi wa polisi wa
kimataifa Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari
hilo litarudishwa Nairobi.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana. Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu
alikanusha habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi
wa Rais Kenyatta bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi.
Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi
aliyeripoti kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa
huyo wa polisi pia alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi
wa Rais.
Tukio
la wizi wa gari hilo, lilisababisha
taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari ya ulinzi wa
Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi mkali. Takwimu za polisi
zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi
kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.
No comments:
Post a Comment