Mtoto Sauda Mohamed aliyeokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake.
MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika.
Habari zinasema mtoto huyo baada ya kuokotwa alifikishwa katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala ambako alipokelewanakulelewa.ALIVYOOKOTWASauda
aliokotwa na msamaria mwema maeneo ya Buguruni sehemu ya wazi akiwa na
umri wa miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye
hajafahamika.
Chanzo
chetu kilisema mara baada ya kuokotwa taratibu zilifanyika kwa
kumfikisha Kituo cha Polisi Buguruni kisha akapelekwa moja kwa moja
katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika
mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo, Dar.
Akifafanua kuhusu
tukio hilo mkurugenzi wa kituo hicho, Mwanaisha Magambo alikuwa na haya
ya kusema: “Sauda aliokotwa akiwa na umri wa miaka mitatu hata hivyo,
walifanya vipimo vya kitaalamu ili kujua umri kwa kumpima kichwa na
baadhi ya viungo vya mwili wake.
“Alipookotwa alikuwa
na hali mbaya sana kipindi hicho kwani alilazwa mwezi mzima katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapumlia mashine na mapigo ya
moyo yalikuwa juu sana.
AGUNDULIKA MATUNDU KATIKA MOYO
“Kutokana na kuwa na hali mbaya, madaktari pale Muhimbili baada ya vipimo wakagundua kuwa ana matundu “Baada
ya kugundulika tatizo alipewa dawa za kutumia na akaruhusiwa lakini
hali ilibadilika na ikalazimu arudishwe tena Muhimbili ambako amelazwa.”
Mtoto Sauda Mohamed akiwa amelala.
MAANDALIZI YA SAFARI YA INDIA
Magambo alisema kuwa
kutokana na maradhi hayo Sauda hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea,
akitaka kusogea huwa anatambaa.“Mbaya zaidi ugonjwa huo umemfanya Sauda
asiwe na uwezo wa kusema na mwili wake umedhoofu ikiwemo miguu.
“Kuna maandalizi
yanafanywa ili apelekwe India kwa matibabu zaidi kutokana na ukweli
kwamba tatizo lake ni kubwa maana sasa hata kula hawezi,” alisema.
Hata hivyo, wakati
tunakwenda mitamboni, mlezi wa mtoto huyo, Bi. Magambo alisema amefariki
dunia na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar.
No comments:
Post a Comment