Tuesday, September 16, 2014

MTOTO HUYU, MAMA YAKE AMTUPA, KISA MGONJWA!


 
Mtoto Sauda Mohamed aliyeokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake.
 MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika.

Habari zinasema mtoto huyo baada ya kuokotwa alifikishwa katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala ambako alipokelewanakulelewa.ALIVYOOKOTWASauda aliokotwa na msamaria mwema maeneo ya Buguruni sehemu ya wazi akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye hajafahamika. 

Chanzo chetu kilisema mara baada ya kuokotwa taratibu zilifanyika kwa kumfikisha Kituo cha Polisi Buguruni kisha akapelekwa moja kwa moja katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo, Dar. 


Akifafanua kuhusu tukio hilo mkurugenzi wa kituo hicho, Mwanaisha Magambo alikuwa na haya ya kusema: “Sauda aliokotwa akiwa na umri wa miaka mitatu hata hivyo, walifanya vipimo vya kitaalamu ili kujua umri kwa kumpima kichwa na baadhi ya viungo vya mwili wake. 

“Alipookotwa alikuwa na hali mbaya sana kipindi hicho kwani alilazwa mwezi mzima katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapumlia mashine na mapigo ya moyo yalikuwa juu sana. 

AGUNDULIKA MATUNDU KATIKA MOYO
“Kutokana na kuwa na hali mbaya, madaktari pale Muhimbili baada ya vipimo wakagundua kuwa ana matundu “Baada ya kugundulika tatizo alipewa dawa za kutumia na akaruhusiwa lakini hali ilibadilika na ikalazimu arudishwe tena Muhimbili ambako amelazwa.”

 
Mtoto Sauda Mohamed akiwa amelala.

 MAANDALIZI YA SAFARI YA INDIA
Magambo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo Sauda hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea, akitaka kusogea huwa anatambaa.“Mbaya zaidi ugonjwa huo umemfanya Sauda asiwe na uwezo wa kusema na mwili wake umedhoofu ikiwemo miguu.

“Kuna maandalizi yanafanywa ili apelekwe India kwa matibabu zaidi kutokana na ukweli kwamba tatizo lake ni kubwa maana sasa hata kula hawezi,” alisema.
  Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, mlezi wa mtoto huyo, Bi. Magambo alisema amefariki dunia na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar.

Monday, September 15, 2014

RUNGWE UCHUMI WAKE UMEJIFICHA HAPA

IMEELEZWA kuwa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeshindwa kupaa kiuchumi kutokana na kushindwa kutumia fursa ya kuvitangaza vivutio vilivyopo ambavyo havipatikani duniani kote vitakavyopelekea wilaya hiyo ipae kiuchumi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na katibu mkuu wa Christian and Gospel Ministry (CGM)wilayani humo Watson Pamesa wakati wa makabidhiano ya jengo la kufungia mitambo kwa ajili ya matumizi ya Redio Rungwe inayotarajiwa kufunguliwa siku za hivi karibuni.

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=1486f81ed9967800&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_i010jhi70&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410781737480&sads=oFsSPQUgvHJmIU-xa2y5Vy_djRc
Makabidhiano hayo ya jengo la ngazi moja yalifanyika jana baada ya uongozi wa Christian kuketi na wakuu wa idara kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Veronika Kessy ambapo mapendekezo na muhtasari wa kikao hicho yatapelekwa kwenye kikao cha baraza la madiwani Agosti 26 mwaka huu kujadiliwa.

Pamesa alisema waliiandikia halmashauri hiyo barua ya kutaka kukodi jengo kwa matumizi hayo yenye kumb,RDC/E.1/117/97 ya tare,07/8/2013 ambapo ilijibiwa na kusainiwa na kaim mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elias Sangi kwa barua yenye kumb,TKY/7.6/VOL.010/2014 ya Tar,30/05/2014 kuwa ombi lao limekubaliwa.

Alisema baada ya makubariano hayo siku ya alhamisi ya tare,11/9/2014 walienda kuoneshwa jengo pamoja na mapendekezo ya ulipaji na kuwa kinachosubiriwa ni maamuzi ya madiwani ambapo wataketi siku hiyo na kutoa maamuzi.

Alivitaja vivutio hivyo ambavyo havipatikani Duniani kote kuwa ni Vinyonga na  Nyani wekundu waliopo mlima Rungwe,daraja la mungu,ziwa ngozi na kisiba wenye ambayo maji yake hayajai wala hayakauki,mti Rungwe ambao jina la wilaya limetokana na mti huo na unatibu magonjwa zaidi ya 45.

Alisema ujio wa redio hiyo utavitangaza vivutio hivyo na kupelekea watalii kuzuru wilaya hiyo na kujionea maajabu ambayo hayapatikani Duniani kote na kuwa wilaya hiyo itakuwa haishikiki kiuchumi kuliko ilivyo sasa ambapo ni ya pili kutoka mwisho kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Christian and Gospel Ministry wilayani humo Amoni Mwakilomo mbali na kuipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwaunga mkono pia amesema mchakato wa redio umefikia ukingoni na sasa wanajipanga kuanzisha gazeti kwa lengo la kutoa huduma ya kihabari kwa wanarungwe.

Chrispin Meela mkuu wa wilaya hiyo alisema watakuwa bega kwa bega na mtandao huo ili kuhakikisha wilaya hiyo inatumia Digital na kuondokana na analojia kwa kuuhabarisha umma kwa matukio mbalimbali na kukuza pato la ndani nje wilayani humo.

KIJANA ALIYEKUFA KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA SHINYANGA AFANYIWA UCHUNGUZI NA MADAKTARI



Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia JANA katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

MAGUNIA MAWILI YA MAHINDI NA SUFURIA NNE YAFANYA WANUSURIKE KUCHUNGULIA JEHANAMU, RUNGWE,….

Watu wawili ambao ni wakazi wa kijiji cha  Kandete Wilayani Rungwe mkoni Mbeya  wamenusurika kifo baada  ya kuambualia  kipigo kikali  kutoka kwa  wananchi  wenye  hasila  kari   baada  ya  kukamatwa  na tuhuma   za  kuboma  ofisi kwa  kuiba mahindi   ya shule    ya msingi  kisalala.
 Wakizunguza kwa masikitiko makubwa  na    yetu lungwe   blog wananchi hao wamesema hatua  hiyo imekuja  kufuatia   vijana  hao kuiba  mahindi na vyombo  vya   shule ambavyo kwa  juhudi  zao wali jichangisha kwa  madhumuni  ya   kuwawekea watoto wao hazina  ya  chakula ambacho kilikuwa  kinatumiwa wakati  wamchana  pindi wakiwa njaa

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148747e14ae362f4&attid=0.7&disp=inline&realattid=f_i02g6tod6&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410780214004&sads=XGvg9OngA3Zk9ZQz-MshEVsCgGg



   Hata hivyo  taaarifa  za awari  kutoka kwa wananchi hao zilieleza  kuwa  katika siku za  hivi karibuni  uongozi wa shule  hiyo uliitisha   kikao  maalmu  kilicho jumuisha wazazi na  walezi   ambapo kupitia kikao hicho waliafikiana kuchangia   mahindi  kilo tano kwa kila mmoja ambazo   zilitolewa na kufanikiwa kununua masufuria manne    kwa ajili   ya  kuwapikia chakula  watoto  wao pindi wakiwa shule.
   Walisema  walishangaa  baada  ya  vijana  hao kujichukulia uamzi mgumu wa kubomoa   ofisi ya  shule na  nyumba  ya mkuu wa shule kwa  kutokomea na vitu  hivyo  ambavyo waliweza kuvikamata  baada ya msako mkali kupita kijijini  hapo.

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148747e14ae362f4&attid=0.4&disp=inline&realattid=f_i02g6tm43&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410780553901&sads=lU-Y7AAGlGl2W2vl9BB1cGDj6c4
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148747e14ae362f4&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_i02g6tlf2&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410780548483&sads=4KGCJv6Di7inRWbCz3Ev1dY1z6o
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148747e14ae362f4&attid=0.10&disp=inline&realattid=f_i02g6tql9&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410780606263&sads=aO9Iz8_VoGs9Gopr3tVNDvCGjOs

  mwenyekiti  wa kamati ya  shule  hiyo, fred  ngiluke mwandimila  alisema   vijana   hao walibomoa  mlango   na kufanikiwa  kuiba gunia  mbili za  mahindi na  masufulia manne ya   kupikia chakula  na  kwamba kutokana  na  hali  hiyo kutokea waliamua kutoa  taarifa    katika  uongozi  wa  kijiji ambao  ulifika  na kuwakamata  mapema

 

   Afisa mtenda wa kata  hiyo  Huluma mwakyusa alikili kutokea kwa  tukio hilo na kwamba watuhumiwa  wamepelekwa  katika  hospitali  ya  wilaya  ya Rungwe yaani   makandana   na huku  wakiwa chini ya   ulinzi  wa  jeshi la polisi na kuwataja  watuhumiwa   hao kuwa ni  Sauli  mwakyage miaka {30}  na   tumaini mwasimbega  mika {35}wote wakiwa  ni  wakazi wa kijiji hicho.
 Kwa upande wa  walimu wa shule  hiyo  akiwamo  Elieza anangisye  walisema    kutokana  na hali  hiyo imepelekea wanafunzi  wao  kushindwa  kupata  chakula   kwa wakati  na ukilinganisha kuwa    vyakula vyote   huwa  vinatolewa na   wazazi na walezi Ikiwa ni pamoja  na wanafunzi   kushindwa  kwenda shule  kutokana   na msako wa   vyakula  kuchukua nafasi yake..
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148747e14ae362f4&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_i02g6tkt1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410780150940&sads=FMJmGsbinU8XcZKGZVEwyUgCsoM

ASKARI JWTZ WAFANYA UNYAMA WALAZIMISHA VIJANA 11 KUNYWA MAJI YENYE KINYESI


Katika  hali isiyo ya kawaida, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanadaiwa kuwafanyia ukatili mkubwa vijana 11, wakazi wa eneo la Keko Magulumbasi B, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kwa kuwapiga na kuwalazimisha wanywe maji machafu yenye kinyesi.

Tukio hilo ambalo limefananishwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, linadaiwa kutokea Septemba 12 mwaka huu, saa 11 jioni, katika eneo la Keko Magulumbasi B.

Inadaiwa kuwa, wanajeshi hao ambao walikuwa saba wakiwa na sare za jeshi hilo, walifika Keko Magulumbasi B wakiwa na kijana mmoja mwenye asili ya Kiarabu na kuwavamia vijana waliokuwa wakila chakula kwenye kibanda cha chipsi.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, wanajeshi hao waliwakamata vijana hao na kudai wanahusika kupora simu ya kijana mwenye asili ya Kiarabu aina ya Tecno yenye thamani ya sh. 25,000.

Pamoja na vijana hao kukataa kuhusika na tukio hilo, waliwekwa chini ya ulinzi, kufungwa mikono kwa kamba, kulazwa kifudifudi na kuanza kupigwa mikanda ya jeshi.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa, vijana hao walichukuliwa hadi kwenye bwawa la maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi cha binadamu wakazamishwa vichwa vyao ndani ya bwawa hilo la kulazimishwa kunywa maji hayo.

Waliongeza kuwa, vijana hao wakiwa wamelowana kwa maji machafu walichukuliwa na wanajeshi hao hadi Kituo Kidogo cha Polisi Keko na kuswekwa rumande na mmoja wao aliachiwa baada ya dakika 10.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walilazimika kuvamia kituo hicho na kufanya vurugu wakiwarushia mawe askari wa kituo hicho kwa lengo la kuwatoa vijana hao kwa nguvu wakidai wameonewa.

Hata hivyo, wananchi hao walitawanywa kwa risasi za moto zilizopigwa hewani na askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Chang'ombe walioitwa kuongeza nguvu kituoni hapo.

Bw. Omary Abdu (30) ambaye ni mkazi wa eneo hilo ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, alidai kutofurahishwa na kitendo kilichofanywa na wanajeshi hata kama vijana hao wameiba kwani walipaswa kufikishwa katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

"Walichokifanya wale wanajeshi ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu...naamini wanafahamika, itakuwa vizuri kama watachukuliwa hatua za kisheria," alisema.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliwashutumu wakazi wenzake kwa kitendo cha kuvamia Kituo cha Polisi na kufanya fujo kwa kuwarushia mawe polisi.

Katika hatua nyingine, mkazi huyo alimtuhumu Mwenyekiti wa Mtaa wa Magulumbasi B, Bw. Mohamed Fundi ambaye alidai kupitia kikao chake na wananchi Agosti 29 mwaka huu, alihamasisha wagome kukamatwa na polisi.

Alidai kauli kama hiyo inaweza kuleta vurugu na uvunjifu wa amani hivyo zinatakiwa kukemewa na kila mkazi wa eneo hilo.

Mwandishi  alimtafuta Bw. Fundi ambaye alikiri kufanya kikao na wananchi kwa tarehe hiyo ambacho kilikuwa na lengo la kuhamasisha maendeleo na kuwafahamisha wananchi haki zao si kuhamasisha vurugu au kuzuia wasikamatwe na polisi kama inavyoelezwa.

Alisema miongoni mwa haki hizo ni namna polisi anavyotakiwa kumkamata raia na asikamatwe usiku bila kuwepo kwa kiongozi wa eneo lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akidai taarifa alizonazo ni kwamba, vijana waliokamatwa wanajihusisha na wizi wa mifukoni.

Alisema wakiwa Kituo Kidogo cha Polisi Keko, wananchi walikivamia na kufanya vurugu hadi walipotawanywa na askari kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Chang'ombe kwa kupiga risasi hewani.

"Taarifa zinazosema vijana hao waliteswa na kunyweshwa maji machafu na wanajeshi bado sijazipata ila hawa vijana wanashikiliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe wakisubiri kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika," alisema.

Inaelezwa kuwa, wiki moja iliyopita kijana huyo mwenye asili ya Kiarabu mkazi wa Keko Toroli, alivamiwa na vijana eneo la Keko Magulumbasi B, ambao walimpora simu ya mkononi tukio ambalo liliripotiwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Keko.

CHADEMA YAPATA SAFU MPYA YA UONGOZI, FREEMAN MBOWE AREJEA KATIKA KITI CHA UENYEKITI KWA KISHINDO.



Uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA umemalizika hapa katika ukumbi wa mliman city ambapo mwenyekiti wake FREMAN MBOWE ameshinda tena kiti hicho kwa kishindo na kutangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa miaka mingine mitano
 

Mtokeo ni kama ifuatavyo
NAFASI YA UENYEKITI---
FREMAN MBOWE---KURA --789
GAMBARANYERE MWANGATEKA---KURA--20

NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI BARA
PROFESA ABDALA SAFARI---KURA--775

NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBAR
SAID ISSA MOHAMED---KURA--645
HAMAD MUSSA YUSUPH--163.



Hivyo aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo ALEX KISURURA amemtangaza mh FREMAN MBOWE kuwa mwenyekiti huku PROFESA SAFARI akichukua nafasi ya makamu mwenyekiti upande wa bara na SAID ISSA MOHAMED kuchukua nafasi ya makamu mwenyekiti upande wa zanzibar.

CHINI KUNA PICHA ZA BAADA YA USHINDI





KIJANA MWENYE AKILI KULIKO WOTE DUNIANI

Terrence Tao, He is a mathematician of Australian and American roots. If you think that math is hard enough, just take a peek into the subfields that Tao is involved with: additive combinatorics, analytic number theory, ergodic Ramsey theory, harmonic analysis, partial differential equations and random matrix theory.
A recipient of the Fields medal in 2006, Tao holds the James and Carol Collins chair in mathematics at the University of California, Los Angeles. He has had good training, learning math when he was barely a toddler, solving arithmetic problems at two years old, studying college level math at nine and getting a gold medal in the international math Olympiad when he was 13. He got his PhD when he was only 20 from Princeton and became a full professor at UCLA when he was 24. He has already published 230 research papers.