DA!
Duniani kuna mambo jamani! Katika hali isiyo ya kawaida, maeneo ya
Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji hawakuamini macho yao wakati
walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29) (pichani), akirejea
nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba moto na
waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia
‘kifo’ chake.Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana
wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja
na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.Iko
hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi
Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi
wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini,
akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale
kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili
kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili
bila mafanikio.
Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka yake na baba yake mzazi
walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa chumba cha kuhifadhia
maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio vikaibuka kwani
wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na kitu kizito
kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.
Ndugu hao walitoka na vilio hadi nyumbani na msiba ukawekwa kwa
kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku sehemu ya kuzikia
makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku ndugu walio
mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.
Siku ya tukio, watu wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya
kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na kusababisha tafrani
kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu wakishangaa
iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa sauti
kuwa, hakufa, alikuwa polisi.
Akizungumza na Uwazi huku akifakamia msosi kwa madai kuwa hakula
tangu alipokamatwa, Fido alisema alikamatwa na polisi lakini akakosa
njia ya kuwasiliana na familia yake.
Naye mke wa marehemu alipopewa nafasi ya kusema alikuwa na haya:
“Nimepigwa butwaa, siamini kama ndiye huyu mume wangu, watu
wamekusanyika kwa ajili ya maombolezo, nilijua hatukonaye tena. Ama
kweli Mungu mkubwa, nimefurahi kufika kwake nyumbani.
“Ilikuwa Jumatano saa 1.45 asubuhi mume wangu aliniaga na kwenda
kazini kwake lakini hadi saa mbili usiku alikuwa hajarudi na si kawaida
yake, ilikuwa nikipiga simu yake inaita tu.
“Ilibidi niende Tandale wanakohifadhia pikipiki, nilikuta wenzake
wamesharudisha pikipiki lakini yeye alikuwa bado.“Tulifuatana na ndugu
zangu hadi Lumumba hatukumuona, tulienda Kituo cha Polisi Msimbazi,
Central, Oysterbay na Kawe lakini walituambia hakuna mtu mwenye jina
hilo aliyekamatwa ama kupatwa na tatizo, ilibidi twende Hospitali ya
Mwananyamala mochwari kuulizia kama kuna maiti iliyookotwa.
“Uongozi wa mochwari ulitueleza kuna maiti tatu zilizopelekwa na
polisi lakini hazifahamiki, moja ni kwa ajali ya pikipiki, mwizi kuuawa
na wananchi na nyingine kuokotwa ufukweni mwa bahari ikiwa imefungwa
kamba mikononi na kukatwa panga kisogoni.
“Mimi, baba pamoja na shemeji yangu tuliingia mochwari kuthibitisha.
Tulipofika katika maiti iliyofungwa kamba na kukatwa panga kisogoni wote
tulijiridhisha kuwa ndiye yeye kutokana na alama alizokuwa nazo,
sikujua kilichoendelea, naamini nilipoteza fahamu baada ya kuuona mwili
huo.
“Tulirudi nyumbani kuandaa msiba, kuweka maturubai, kununua sanda na
kuandaa jeneza, tulipiga simu sehemu mbalimbali hadi mikoani kuwajulisha
ndugu.“Tulijiandaa ili ndugu wa Morogoro na mikoa mingine wakija katika
mazishi yaliyotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (iliyopita) katika
makaburi ya hapa Tandale ambapo tulishapewa eneo la kuchimba kaburi.
Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa akila.
“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi waombolezaji kwa usumbufu,
baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine waliendelea kuwepo hata
ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na Mtwara.
Credit:GPL
No comments:
Post a Comment