Mwanamke anayedaiwa kuwa mchawi akiwa amedondoka Kanisani.
NI
kweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries
lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa
mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa
kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi hayo, Nabii Gideon
Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea mambo ya ajabu
kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa
saba usiku mwanamke huyo akiwa na wenzake watatu, walidondokea kanisani
hapo na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi
ndani. Mwanamke huyo alikuwa na kitambaa chekundu kikidaiwa ni hirizi,
fimbo nyeusi iliyozungushiwa shanga na alikuwa amejipaka masizi
mwilini.
Mwanamke baada ya kudondokea kanisani na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani.
Akizungumza
na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao walidondoka watatu, wawili
walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja aliyejitambulishwa kwa jina
moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A jijini Dar.
Baada ya tukio hilo
vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na polisi walifika kwa lengo la
kuhakikisha usalama wa eneo hilo lakini nabii huyo aliomba mtu huyo
asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi maalum.
Ombi la kiongozi huyo
lilikubaliwa ambapo Aisha alipandishwa madhabahuni na kukiri kuwa
alikuwa na wenzake watano lakini katika kuanguka walikuwa watatu, wawili
walifanikiwa kukimbia bila kusema walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.
Kitambaa chekundu alichokuwa nacho mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”
No comments:
Post a Comment